[theme_section_hidden_section.ReportAbuse1] : Plus UI currently doesn't support ReportAbuse gadget added from Layout. Consider reporting about this message to the admin of this blog. Looks like you are the admin of this blog, remove this widget from Layout to hide this message.
Umati mkubwa wa mahujaji wa Kihindu umekusanyika nchini India na kuoga katika maji wanayoamini kuwa matakatifu Jumatatu katika wa ufunguzi wa tamasha la ibada linalofahamika kama Kumbh Mela.
Waandaaji wa tamasha hilo wanatarajia watu milioni 400 watashiriki kwenye kusanyiko hilo kubwa zaidi kuwahi kutokea.
Tamasha la kidini la Wahindu linalohusisha ibada ya kuoga linafanyika katika eneo inapokutana mito mitatu, Ganges, Yamuna na Saraswati.
Waziri Mkuu wa India Narendra Modi ameliita kusanyiko hilo kuwa "tukio takatifu" linalounganisha pamoja watu wengi katika imani, ibada na utamaduni. Naye Waziri kiongozi wa jimbo la Uttar Pradesh Yogi Adityanath, amewakaribisha mahujaji kwenye tamasha alililota kuwa kubwa zaidi la kiroho na kiutamaduni.
Wakati wa kuanza kwa tamasha hilo, watawa wa Kihindu wameonekana wakiwa wamebeba bendera kubwa za madhehebu yao wakati matrekta yakikokota sanamu za miungu ya kihindu na kusindikizwa na tembo. Mahujaji waliojitokeza kwa wingi wamesikika wakipiga ngoma pamoja na honi kama sehemu ya ibada yao.