[theme_section_hidden_section.ReportAbuse1] : Plus UI currently doesn't support ReportAbuse gadget added from Layout. Consider reporting about this message to the admin of this blog. Looks like you are the admin of this blog, remove this widget from Layout to hide this message.
Jimbo la Lose Angels nchini Marekani limeendelea kuteteketea kwa moto ambao ulizuka usiku wa kumkia januari 9 2025 huku ajali hiyo ikiendelea kusababisha vifo na kuharibu miundombinu
Taarifa ya mchunguzi wa kiafya wa jimbo hilo, imesema mpaka sasa vimeshatipotiwa vifo zaidi ya kumi na miili hiyo inasubiri kutambuliwa kisheria na ndugu zao.
Mapema jana, Rais Joe Biden alisema kuwa moto huo unaowaka katika eneo la Greater Los Angeles, ulikuwa mbaya zaidi kuwahi kushuhudiwa katika historia ya jimbo hilo la magharibi mwa Marekani.
Biden amesema watu 360,000 wameondolewa hadi sasa. Hata hivyo, chanzo cha moto huo bado hakijajulikana.
Maelfu watumwa kuukabili moto wa nyika Californiaulingana na Mkuu wa Kikosi cha Zimamoto cha Los Angeles, Kristin Crowley, zaidi ya nyumba 5,300 zimeharibiwa katika kitongoji cha Pacific Palisades peke yake tangu siku ya Jumanne.
Aidha, Takribani majengo 4,000 hadi 5,000 yameungua au kuteketea kabisa katika eneo la Eaton Fire karibu na Pasadena.