NETANYAHU NA BIDEN PAMOJA KUZUIA VITA YA ISRAEL NA GAZA

Bruno Kaitaba


 Waziri Mkuu wa Israel Benjamin Netanyahu na Rais wa Marekani Joe Biden wamezungumza kuhusu juhudi za kufikiwa makubaliano ya kusitisha mapigano Kati ya Israel na Ghaza

Juhudi hizo zinafanyika zikiwa zimebaki siku chache kabla ya rais mteule wa Marekani Donald Trump hajaingia madarakani wiki ijayo.

Wapatanishi Marekani, Qatar na Misri wamekuwa kwenye mazungumzo juu ya kusitishwa mapigano tangu mwaka uliopita bila mafanikio lakini mara hii maafisa wa Marekani wamesema wanayo matumaini ya kufikiwa makubaliano.

Mkuu wa shirika la ujasusi la Israel (Mossad) David Barnea na mshauri mkuu wa Rais Biden kuhusu masuala ya mashariki ya kati Brett Mc Gurk, wako mjini Doha, Qatar kwa mazungumzo.

Post a Comment

Oops!
It seems there is something wrong with your internet connection. Please connect to the internet and start browsing again.
AdBlock Detected!
We have detected that you are using adblocking plugin in your browser.
The revenue we earn by the advertisements is used to manage this website, we request you to whitelist our website in your adblocking plugin.