[theme_section_hidden_section.ReportAbuse1] : Plus UI currently doesn't support ReportAbuse gadget added from Layout. Consider reporting about this message to the admin of this blog. Looks like you are the admin of this blog, remove this widget from Layout to hide this message.
Operesheni za uokozi zilianza tena leo kuwafikia watu zaidi ambao huenda bado wamekwama mgodini humo.
Kiongozi wa jamii ya eneo hilo, Johannes Qankase, amesema wachimba Mgodi waliookolewa ni wamedhoofika mno na wana upungufu wa maji mwilini.
Amesema wengi wao wamepelekwa hospitali wakati wawili wanaaminika kuwekwa kizuizini na polisi.
Maafisa wa serikali wanatarajiwa kulitembelea leo eneo hilo la mgodi huku shughuli ya uokozi ikiendelea.
Operesheni hiyo inafuatia sakata ya wiki kadhaa kwenye mgodi huo uliotekelezwa, ambapo maafisa wanatuhumiwa kwa kujaribu kuwalazimisha wachimbaji hao kujitokeza nje kwa kuzuia chakula na maji kuteremshwa kwao na jamii ya eneo hilo.
Haijulikani wazi ni watu wangapi waliobaki kwenye mgodi huo. Serikali imesema jana kuwa zaidi ya watu 1,000 wanaohusika na uchimbaji haramu wa madini katika eneo hilo wametoka mgodini na kukamatwa mpaka sasa.